Huyu mtoto ameokotwa Mitaa ya Bamaga anajitambulisha kama Abigael lkn hajui jina la mama wala baba wala sehemu anakoishi kwa sasa yupo Parokiani Maximilian Kolbe, Mwenge. Mwenye kumfahamu afike Parokiani mara moja, naomba tusambaze ujumbe huu kwenye majukwaa mbalimbali, ahsante!
UPDATE: WAZAZI WAMEMPATA MTOTO Baba yake ndio huyo hapo, kweli mitandao ina faida kubwa ya kufanya Dunia kuwa Kijiji. Hebu angalia sasa, familia inafuraha tena. Ahsanteni nyote!❤️🙏
@DrWinnie01 Wazazi tuwe tunawafundisha watoto majina yetu sisi , watoto wanashika vizur tu hata akiwa na Miaka miwili .
@DrWinnie01 Jamani tufundishe Watoto wetu kujua Jina la Baba, jina la Mama, ikibidi jina la Mjumbe na kama ni kwanafumzi mwandikie namba za simu ya Baba, Mama au Mjumbe kwenye madaftari yake yote ukurasa wa mwisho nyuma ya madaftari yake yote. Pia tuwafundishe kujua Jina la mtaaa anaoishi🙏
@DrWinnie01 @jeju_julius She's cute like my Abigail jamani ❤️