Jana nilipata wasaa wa kupita Mtaa wa Mombasa, Unguja kuwaona majirani zangu wa zamani Bi. Asha Salum na mumewe, Inspekta Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Rashid Zam Ali. Kushoto ni bintiye Bi. Asha pamoja na mjukuu wao. Bi. Asha nilisoma naye darasa moja shule ya msingi na shule ya sekondari kati ya mwaka 1969 hadi mwaka 1973, idadi ya wanafunzi wa kike katika shule zetu nchini ikiwa chini ya asilimia 20. Kote ninapopita katika nchi yetu naona hatua kubwa tuliyopiga kielimu, tukiishi maneno ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere ya kwamba kwa watu masikini kama sisi, elimu inapaswa kuwa chombo cha ukombozi, na ukitaka kumsaidia masikini somesha watoto wake. Nafarijika kwamba nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kuongeza fursa za elimu hasa kwa mtoto wa kike, na sasa tuna mgawanyo wa darasa kijinsi wa karibu nusu kwa nusu katika maeneo mengi nchini. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, tumeifanya vyema kazi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo madarasa zaidi ya 20,000, na nina imani kwamba kazi inayoendelea ya kuleta ubora na tija zaidi katika mfumo wetu wa elimu itafanikiwa.
@SuluhuSamia Shikamoo mama,, Iran na Israel wanakiwasha uko na sisi tufanye tuwachokoze wakenya tuwawashie moto tutest vyombo vyetu viache kuota kutu kule kambini 🤓
@SuluhuSamia Jina lako linaakisi matendo na kazi zako. #mamaanafanikisha
@SuluhuSamia Sina la kuongeza hapo Rais Samia Suluhu Hassan. Ninakubaliana nawe asilimia 150%✅! Ukombozi wetu kama Waafrika utatokana na kuwaelimisha watoto wetu wote wa kike na kiume. Asanteni sana kwa kazi yako 🙏🏽🙏🏽
@SuluhuSamia Mama naomba ata 5M nijikwamue kimaisha maana tunaambiwa tujiajiri lakini vyanzo vya kujiajiri tunavyo ili mitaji hatuna.
@SuluhuSamia Majirani zangu waishi na mimi vizuri sasa maana hawajui kesho nitakuwa nani😎
@SuluhuSamia Kazi unayoifanya inaonekana kila kona, watanzania wanaona kwamba #mamaanafanikisha maisha bora.